Top Stories

Maparachichi ya afya zaidi yagunduliwa Hispania

on

Kutokana na tunda aina ya parachichi kuelezwa na wataalamu wa afya kuwa lina mafuta mengi yanayoweza kunufaisha mwili, wataalamu hao hao pia wametengeneza aina ya kuotesha maparachichi ambayo yana mafuta kidogo kuliko maparachichi mengine.

Aina hii ya maparachichi yatakua na asilimia 70 tu ya mafuta tofauti na maparachichi ya kawaida na hii ni kwaajili ya kusaidia watu wenye matatizo ya mafuta mwengi mwilini ambao wanaogopa kutumia tunda hilo kabisa.

Kwasasa maparachichi hayo yanapatikana nchini Hispania na inaelezwa kuwa hivi karibuni yataanza kusambazwa maeneo mbalimbali duniani. Maparachichi haya mapya yanaelezwa kuwa mepesi kwa uzito na yana afya zaidi kwani hapunguza viwango vya mafuta mabaya mwilini.

Ulipitwa na hii? Rais JPM: “Kama Aga Khan imesamehewa kodi, mbona gharama za huduma bado ziko juu?”

Soma na hizi

Tupia Comments