Michezo

Historia nyingine ya Harry Kane ya kusisimua

on

Jina la nahodha wa timu ya taifa ya England anayecheza club ya Tottenham Hotspurs ya England Harry Kane ana historia ya kuvutia katika maisha yake.

Miaka 13 iliyopita Harry Kane ambaye kwa sasa ni nahodha wa England alikuwa na ndoto ya kukutana walau kupiga picha na staa wa England wa wakati huo David Beckham lengo ambalo alilitimiza.

Usiku wa July 3 2018 Harry Kane anaweka historia ya kuwa nahodha wa kwanza kuwahi kuiongoza England World Cup katika mikwaju ha penati na kushinda dhidi ya Colombia, hiyo ni baada ya dakika 120 kumalizika matokeo yakiwa 1-1 ndio England akapata ushindi wa penati 4-3.

Katika picha inayosambaa mtandaoni ya story ya kuvutia ya Harry Kane akiwa na David Beckham ni kiwa aliipiga picha miaka 13 iliyopita akiwa yeye, mchezaji mwenzake wa kike na Beckham lakini leo Kane amekuwa staa na yule mchezaji wa kike waliopiga picha na Beckham miaka hiyo amekuwa mkewe.

 

Soma na hizi

Tupia Comments