Top Stories

Emerson kaeleza jinsi Hazard alivyojitoa kwenye group la whatsapp la wachezaji wa Chelsea

on

Ni wiki moja imepita toka club ya Real Madrid ya Hispania itangaze rasmi kukamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji aliyekuwa anaichezea Chelsea Eden Hazard.

Hazard amejiunga na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano ambapo dau la usajili linatajwa kuwa zaidi ya pound milioni 80 ndio zimetumika kumng’oa Hazard Stamford Bridge.

Leo Emerson ameeleza kuwa Eden Hazard aliyedumu na timu hiyo kwa miaka 7 ameshitushwa na uamuzi wake wa kuamua kujitoa kwenye group la whatsapp la wachezaji wa Chelsea.

“Alituma tu ujumbe kwenye group la whatsapp na kuandika ‘Asanteni na nawapenda’ halafu aka-left group nikasema daa kweli ame-left”>>>> Emerson

Soma na hizi

Tupia Comments