Michezo

Simba yakutana na wababe wao Mwadui FC

on

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC hatimae wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu msimu wa 2019/2020 dhidi ya Mwadui FC.

Simba SC baada ya kucheza michezo sita bila kupoteza Simba SC leo imepoteza kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Goli la Mwadui FC lilifungwa na Gerald Mathias dakika ya 32, Simba SC anaendelea kuwa kileleni kwa kuwa na point 18, huku golikipa wao Aishi Manula akicheza mechi yake ya 100 toka ajiunge na Simba SC akiwa na clean sheet 59 (kucheza mechi 59 bila kuruhusu goli)

Soma na hizi

Tupia Comments