Mix

TOP TEN: Habari 10 ‘HOT’ zilizotikisa wiki hii kuanzia July 10 hadi 15, 2017

on

Mambo mengi yamepita na kujadiliwa sana kwenye mitandao mbalimbali katika nyanja za Uchumi, Siasa, Utamaduni na Jamii huku baadhi yakipewa uzito mkubwa, mengine wastani na mengine hayakutajwa kabisa.

Miongoni mwa stori zilizotajwa sana na kupewa uzito mkubwa ni pamoja na ujio wa Klabu ya Everton ya England ambayo ilicheza dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kufika Makao Makuu ya Polisi kwa mara ya tatu na TRA kuvifungia vituo vya mafuta visivyofuata sheria wakati wa kutoa risiti za kielektroniki.

Kama ulikosa stori hizo au hukuwa na time ya kutosha kuyafuatilia kutokana na pilika za wiki, Ayo TV na millardayo.com zinakupa nafasi ya kuzipitia kwa undani zaidi kwenye hii list ya stori 10 za wiki.

10: Kesi ya James Rugemalira na Harbinder Sethi kuahirishwa baada ya Sethi kuugua.

July 14, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliahirisha kesi inayowakabili James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya upande wa utetezi kusema mmoja wa watuhumiwa hao kutokuwa na afya nzuri kutokana na kusumbuliwa na uvimbe tumboni.

9: Kufungiwa kwa Kampuni ya SAHARA MEDIA ikidaiwa Tsh. Bilioni 4 na TRA

July 13, 2017 Habari kutoka Mwanza zilikuwa ni pamoja na taarifa za kufungiwa kwa Kampuni ya SAHARA MEDIA inayomiliki Star TV, RFA na Kiss FM kwa siku 14 ikidaiwa kodi ya zaidi ya Bilioni 4 na Mamlaka ya Mapato Tanzania‘TRA’. Kodi hiyo wametakiwa kuilipa ndani ya siku 14 na isipofanya hiyo TRA itapiga mnada Kampuni hiyo.

Meneja Rasilimaliwatu wa Sahara, Rafaeli Shilatu alikiri kufungiwa akidai ni kutokana na malimbikizo ya kodi.

8: Maamuzi ya Mahakama kwa Vigogo wa TRA waliodaiwa kuhujumu Bil. 12.7

July 13, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuachia huru aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kusababishia hasara ya Tsh 12.7 bilioni.

Washtakiwa hao waliachiwa huru mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali  Mkuu, Timon Vitalis kuiomba Mahakama iwaachie chini ya kifungu cha 91(1) cha mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.

Wengine walioachiwa huru mbali ya Masamaki wengine ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya, Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan.

7: Tamko la CUF kuhusu hujuma wanazodai kufanyiwa na CHADEMA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Magdalena Sakaya July 12, 2017 alitoa tamko kukemea vikali kinachodaiwa kuwa hujuma za CHADEMA zinazofanywa dhidi ya CUF ili kukiua chama hicho.

6: Kifaa cha kugundua kiwango cha sumu kwenye maji taka kimezinduliwa

Naibu Waziri wa Mazingira Luhaga Mpina July 11, 2017 alifanya ziara katika Mto Msimbazi ambako alizindua kifaa maalumu ambacho kina uwezo wa kugundua pao hapo maji yenye kemikali za sumu yanayotiririshwa kutoka viwandani.

5: Kilichoamuliwa na Mahakama kuhusu kesi ya Halima Mdee

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano July 10, 2017 alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka moja la kumkashifu Rais alilolitenda July 3, 2017 akiwa Makao Makuu ya CHADEMA DSM. Mdee alidhaminiwa na atarejea tena Mahakamani August 7.

Baada ya kuahirishwa kesi hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alifunguka na kuizungumzia issue hiyo.

4: GUMZO LA ESCROW: Sababu 5 za William Ngeleja kurudisha Fedha za ESCROW

July 10, 2017 Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alitangaza kurejesha pesa Tsh. milioni 40.4 za mgawo kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemarila ambaye inaelezwa alilipwa zaidi ya Bilioni 300 za ESCROW.

Ngeleja alizitaja sababu kuu 5 za kurejesha fedha hizo.

3: Wayne Rooney na kikosi cha Everton kuwasili Tanzania kucheza dhidi ya Gor Mahia

July 12, 2017 Klabu ya Everton iliwasili Dar es Salaam ikiwa na wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya. Everton ikiongozwa na staa wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney walipokelewa na Waziri wa Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

2: Lowassa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi DSM

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa July 13, 2017 aliripoti kwa mara ya tatu katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi DSM kwa ajili ya mahojiano akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi wakati wa futari mwezi Mtukufu wa  Ramadhan.

Lowassa aliripoti Makao Makuu ya Polisi saa tatu asubuhi na baada ya takribani dakika 30 Wakili Kibatala alitoka nje na kutoa taarifa kuwa wameambiwa warudi tena Alhamisi ya July 20 mwaka huu.

1: TRA kuvifungulia baadhi ya Vituo vya Mafuta ilivyovifungia DSM

Stori kubwa ambayo inamake headlines kwenye mitandao kwa sasa ni kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kuvifungia vituo vya mafuta ambavyo havifuati utaratibu wa kutoa risiti za kielektroniki kutoka kwenye mashinde zilizofungwa moja kwa moja kwenye pump ‘EFPP’.

TRA imesema zoezi hilo ni endelevu na wataendelea kukagua na kuvifungia vituo vyote ambavyo havifuati sheria na taratibu katika kutoa risiti za kielektroniki mpaka pale wahusika watakapofanya hivyo.

Soma na hizi

Tupia Comments