Michezo

Rais mpya wa CAF ametangazwa leo Addis-Ababa Ethiopia

on

Mkutano wa 39 wa shirikisho la soka barani Afrika CAF leo March 16 2017 ulikuwa unafanyika Addis-Ababa Ethiopia, mkutano huo ambao ulijadili mambo kadhaa ikiwemo kusikiliza ombi la Zanzibar la kutaka kuwa mwanachama rasmi wa CAF, ulifanyika pia uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo.

Ahmad Ahmad

Wagombea wa nafasi za Urais walikuwa ni Rais wa sasa wa shikisho hilo Issa Hayatou na Ahmad Ahmad wa Madagascar, katika uchaguzi huo uliyofanyika leo Ahmad Ahmad amemshinda Issa Hayatou kwa kura 34 wakati Hayatou akiambulia kura 20.

Issa Hayatou

Hayatou anaondoka madarakani baada ya kutawala shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa miaka 27, Issa Hayatou aliingia madarakani mwaka 1988 na ndio Rais wa  CAF aliyetawala muda mrefu zaidi akifuatiwa na Yidnekatchew Tessema aliyetawala miaka 15.

Waliyowahi kuwa Marais wa CAF

  1. Abdel Aziz Abdallah Salem (1957-1958)
  2. Abdel Aziz Moustafa (1958-1968)
  3. Abdel Halim Muhammad (1968-1972)
  4. Yidnekatchew Tessema (1972-1987)
  5. Abdel Halim Muhammad (1987-1988)
  6. Issa Hayatou (1988-2017)
  7. Ahmad Ahmad (2017-)

ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments