Michezo

Mahusiano ya Pogba na Ole Gunnar Solskjaer yanaanza kupotea

on

Ikiwa imepita siku moja toka club ya Man United ipoteze mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League 2018/2019 dhidi ya FC Barcelona, Man United walipoteza kwa goli 1-0 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani goli ambalo lilipatikana mapema mwanzoni mwa mchezo.

Leo zimeripotiwa taarifa kuwa uhusiano kati ya kocha wa sasa wa Man United Ole Gunnar Solskjaer dhidi ya kiungo wake Paul Pogba umeanza kufifia, haupo kama ilivyokuwa awali kutokana na kiungo huyo kudaiwa kushinikiza kuhama Man United mwisho wa msimu, kitu ambacho Ole Gunnar Solskjaer hakubaliani nacho na anadhani kitadhoofisha kikosi chake.

Pogba amekuwa katika list ya miongoni mwa wachezaji watatu wakiwemo Hazard wa Chelsea na Mbappe wa PSG kuhitajika na kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane mwisho wa msimu kitu ambacho kinadaiwa kumvutia sana Pogba, Pogba amekuwa na msimu mzuri chini ya Solskjaer ukilinganisha na Jose Mourinho, katika mechi 12 za mwanzo za Solskjaer ndani ya Man United Pogba alifunga magoli9.

Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys

Soma na hizi

Tupia Comments