Michezo

Man United imekubali Sanchez amfuate Lukaku

on

Club ya Man United ya England leo imeripotiwa kuwa ipo tayari kumuachia mshambuliaji wake wa kimataifa wa Chile Alex Sanchez akaungane na Romelu Lukaku katika club ya Inter Milan ya Italia, Man United wamekubali kumtoa kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua mwisho wa msimua.

Sanchez anaripotiwa kuwa tayari kurudi Italia baada ya kuwa na msimu mbovu katika club ya Man United, vyanzo mbalimbali vinaripoti kuwa pamoja na kuwa Inter Milan wamekubali kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo lakini hawa cha kumu ofa zaidi ya mshahara wa pound 150000 kwa wiki.

Alex Sanchez mwenye umri wa miaka 30 inaripotiwa kuwa Jumatano ya August 28 2019 atakuwa Milan kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kukamilisha uhamisho wake, Sanchez alikataa ofa ya kujiunga na Man City January 2018 na kuamua kujiunga na Man United, uhamisho ambao ulihusisha pesa na kumtoa Henrikh Mkhitaryan kwenda Arsenal.

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments