Michezo

EXCLUSIVE: Sababu iliyopelekea ndege ya TP Mazembe kutua Songwe Mbeya

on

Club ya TP Mazembe kwa sasa ipo Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya wenyeji wao Simba SC, TP Mazembe wamewasili Dar es Salaam jana lakini wakiwa wanakuja Dar es Salaam ndege yao ilitua kwa saa moja katika uwanja wa Songwe Mbeya.

Leo AyoTV imekutana na meneja wa uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya Pius Kazeze na ameeleza sababu zilizopelekea ndege hiyo kusimama kwa saa moja na dakika 5 katika uwanja wa Songwe, ndege hiyo ilikuwa na abiria 29 na wahudumu wa ndege.

“Jana tulipokea ugeni wa ndege iliyotoka Lubumbashi kuelekea Dar es Salaam lakini ilitua kiwanjani hapa kwa lengo la kuongeza mafuta kutokana na ndege hiyo kutokuwa na uwezo wa kusafiri moja kwa moja kutoka Lubumbashi mpaka Dar es Salaam bila kupitia kituo chochote cha kati kati”>>>Pius Kazeze

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments