AyoTV

Uliisikia ya Afrika Mashariki kutumia Mtandao mmoja? ninao ufafanuzi

on

Inawezekana wewe ni mmoja wa Watanzania waliosoma taarifa kwamba Afrika Mashariki inajipanga kutumia mtandao mmoja lakini hujaelewa vizuri mtandao mmoja kivipi na ndio maana AyoTV na millardayo.com zinakukutanisha na Mbunge kutoka bunge la Afrika Mashariki.

Mbunge wa Afrika Mashariki Abdullah Mwinyi amesema ‘maana ya mtandao mmoja ni kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki ina nchi 5, kulikua na mpango wa kufanya mawasiliano ya simu ndani ya jumuiya hii yasiwe na tofauti, yawe kama ya ndani ya nchi maana kwa sasa ukipiga simu nje ya Tanzania unachajiwa zaidi kuliko kumpigia aliyeko Tanzania

‘Sasa tunataka tufanye ONE NETWORK ili gharama iwe moja, Wenzetu walishatangulia na wameshafanikisha hilo, simu ambayo inapigwa kutoka Kenya, Uganda na Rwanda haina tofauti ya gharama…. maana ya mtandao mmoja ndio hiyo na sio kwamba kuna kufuta mitandao mingine alafu tukatumia mtandao mmoja tu wa Vodacom’

Kimsingi wote tumekubaliana hivyo lakini kila nchi itafanya kwa jinsi watavyoona itawasaidia, kipindi kilichopita Tanzania kidogo walikua wazito wakiamini kwamba mapato ya kiserekali yatapungua lakini takwimu zinaonyesha wenzetu waliofanya japokua gharama zimeshuka, wingi wa simu umepanda na hatimae mapato yameongezeka maana watumiaji wameongezeka

ULIPITWA? Tazama Diamond Platnumz alivyojibu maswali ya Waandishi kwenye tuzo za MTV MAMA South Africa, bonyeza play kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments