AyoTV

Ebitoke baada ya kukutana na Ben Pol

on

Mwimbaji wa RnB Ben Pol katika kuthibitisha kuguswa na ombi la mchekeshaji Ebitoke aliyetaka wafunge naye ndoa alipost picha kwenye Instagram yake na kuandika ujumbe wa shukrani kwa kuzipokea hisia zake.

Sasa new story baada ya tukio hilo ni kwamba Ayo TV na millardayo.com zimempata Mchekeshaji Ebitoke kwenye EXCLUSIVE Interview ambapo kaelezea hisia zake baada ya kukutana na Ben Pol.

“Kwanza napenda kumshukuru sana Meneja wangu kwa sababu yeye ndiye alifanya mpaka mimi nikakutana na Ben Pol na pia nimefurahi sana nimekutana na Ben Pol kwa sababu ni ndoto ambayo nilikuwa naisubiria kwa muda mrefu sana. Nimetimiza ndoto yangu na ombi langu.

“Ben Pol ni mtu mzuri kwa ukweli, nilivyokutana naye mwenyewe alifurahi sana. Kuniona mimi ali-appreciate mwenyewe nilifurahi. Alikuwa kwenye furaha ya ajabu ambayo sikutegemea.

“Nilitegemea kwamba nikikutana na Ben Pol atanichukulia sijui mtu gani lakini to be honest Ben Pol kanipokea vizuri sana na pia tumeongea mengi. Nimemuelezea hisia zangu ambazo nilikuwa nazielezea hadharani, ye mwenyewe nimemuelezea. Tumeongea vingi but sitaweza kuvisema vyote.” – Ebitoke.

ON AIR WITH MILLARD AYO: Roma kaeleza kwa nini hayupo tena Instagram huku akitaja mambo matatu kuhusu JPM…bonyeza PLAY kwenye VIDEO hii kutazama!!!

 

Soma na hizi

Tupia Comments