Sierra Leone ni nchi ambayo imepata athari kubwa zaidi kutokana na ugonjwa wa Ebola tangu ugonjwa huo ulipoanza zaidi ya mwaka mmoja sasa, athari yake sio kwa watu waliofariki ama kupata maambukizi ya Ebola pekeyake, imefikia hatua hata ya uchumi wa nchi hiyo kuwa kwenye hali mbaya, shule zimefungwa na vitu vingine vingi kusimama.
Hii sio mara ya kwanza Serikali kutoa agizo kama hili ambalo limetolewa la watu wote kukaa ndani kwa siku tatu kuanzia leo March 27 mpaka Jumapili March 29 ili wafanye ukaguzi wa nyumba hadi nyumba kujua kama kuna watu ambao wana dalili za ugonjwa huo waweze kuwapata na kusaidia watu wengine wasipate maambukizi hayo.
Siku ya Ijumaa zimetolewa saa mbili tu kwa waislamu kwenda kuswali, siku ya Jumapili pia zitatolewa saa tano kwa ajili wakristo kwenda kusali.
Mataifa matatu ya Afrika Magharibi yalioathiriwa vibaya na Ebola ni Sierra Leone, Liberia pamoja na Guinea na zimepanga kuhakikisha zinatokomeza ugonjwa huo ifikapo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook