Mix

Hii ni taarifa kuhusiana na Ebola kupiga hodi nchi nyingine nje ya Afrika.

on

ebola-virus-alert2Taarifa kutoka Australia zinasema mtu mmoja amewekwa katika uangalizi maalumu akifanyiwa vipimo ambapo taarifa za awali zimesema kuwa mgonjwa huyo ana homa na dalili za maambukizi ya Ebola.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 18 amewasili Australia akitokea Guinea siku 11 zilizopita akiwa ameongozana na ndugu zake 8 ambapo walimuweka katika karantini ya nyumbani na baadaye hali yake ilibadilika.

Majibu ya awali ya uchunguzi wa vipimo yanatarajiwa kutoka mapema Jumatatu, na mgoonjwa huyo atafanyiwa vipimo vingine ndani ya siku 3.

Majibu yakionesha ana maambukizi ya ugonjwa huo Australia itakuwa nchi ya tisa kupatikana na mgonjwa wa Ebola tangu iliporipotiwa kuzuka kwa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka huu nchi za Afrika Magharibi, na pia atakuwa ni mgonjwa wa kwanza kuumwa ugonjwa huo Australia.

 

Tupia Comments