Mix

Huyu ndiye mgonjwa wa kwanza kuumwa Ebola kwenye nchi hii.

on

Ebola BillboardSerikali ya Mali imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa na maambukizi ya Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014.

Taarifa kutoka mtandao wa the World Post zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola Afrika Magharibi.

Mali inakuwa nchi ya sita kutangaza kupatikana mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi, lakini ndani ya siku 7 nchi za Senegal na Nigeria zimetangaza kutokuwa na mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola.

Ripoti iliyotolewa na WHO imeonesha vifo zaidi ya 4,900 vimetokea katika nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia.

Timu ya wanasayansi wa kimataifa imejipanga kutafiti uwezekano wa kutumia damu ya mtu aliyewahi kupona Ebola kama tiba ya ugonjwa huo.

Mali inapakana na nchi ya Guinea kwa upande wa Kusini Magharibi, lakini mtoto huyo anakuwa mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini humo.

Tupia Comments