Mix

Sentensi tano za Esther Bulaya kuhusu wanaoweka makalio na maziwa ya bandia… (Audio)

on

youhavebeenwarnedyhbw1

Kwa mara nyingine tena ishu ya vipodozi imeingia kwenye mjadala wa Bunge… May 27 2015 nilikusogezea stori toka Bungeni, Wabunge wakataja majina ya ‘mikorogo’ ambayo sikuwahi kuyajua.

Leo JUNE 09 2015 Mbunge Esther Bulaya kapata kama dakika moja hivi kabla Bunge halijaahirishwa, akatoa sentensi hizi tano kuhusu ishu ya wanawake kutumia makalio na maziwa ya bandia: “Kuna tatizo kubwa limeingia kwa watu kuweka makalio ya bandia na manyonyo bandia.. Tatizo hili ni kubwa, kuna picha zinasambaa kwenye mitandao, athari yake watu wanapata cancer na kuharibika miili yao kutoka majeraha makubwa“>>>

bulaya-akitoa-maoni

Mbunge Esther Bulaya.

Serikali isiangalie suala tu la vipodozi na mikorogo usoni.. hili la watu kuweka makalio na matiti bandia limeingia na linaleta madhara makubwa sana hasa cancer“>>>– Esther Bulaya.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments