Kiungo wa zamani wa Kimataifa wa Ubelgiji na vilabu vya Chelsea ya England na Real Madrid ya Hispania Eden Hazard leo ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 32.
Hazard amesema “Ni lazima usikilize nafsi yako na kustaafu katika wakati sahihi, baada ya kucheza soka kwa miaka 16 na kucheza mechi takribani 700, nimeamua kustaafu rasmi kucheza soka”
“Pia nataka kuzishukuru klabu ambazo nimechezea: LOSC, Chelsea na Real Madrid; na kuwashukuru RBFA kwa Uteuzi wangu wa Ubelgiji.”
“Shukrani za pekee kwa familia yangu, marafiki zangu, washauri wangu na watu ambao wamekuwa karibu nami katika nyakati nzuri na mbaya,” aliongeza.
Hazard amestaafu soka baada ya kuwa na majeruhi ya mara kwa mara na anaacha soka akiwa amecheza jumla ya mechi 749, magoli 200 na mataji 15.