Ad
Ad

Mix

Jux kafunguka kuhusu penzi jipya la Vanessa ‘Nampenda Rotimi nafuatilia tamthilia yake’

on

NI Headlines za msanii kutoka Bongo Flevani, Juma Jux ambae kwasasa yuko nchini Kenya Nairobi kwaajili ya kuitambulisha album yake mpya iitwayo The Love Album aliyoizindua hivi karibuni.

Sasa miongoni mwa maswali aliyokutaka nayo katika kituo cha Radio kiitwacho Kiss FM Nairobi aliulizwa kuhusu taarifa za kuachana na Vanessa Mdee, Staa huyo alifunguka na kusema yeye na Vanessa waliachana mwezi wa 12 mwaka 2018.

Na kwa upande  mwingine Jux alipoulizwa kuhusu Rotimi ambae ndie mpenzi mpya wa Vanessa Mdee alisema ‘Kuna kipindi ambacho nilichokuwa nakisubiria Vanessa Mdee aje kuwa na furaha kwahiyo niwe mkweli nina furaha kingine watu ambacho hawajui mimi ni shabiki wa tamthilia ya Power nakubali uigizaji wake nampenda Rotimi’– Jux

‘Siwezi kudanganya wakati tumegombana tulikuwa sawa hapana kila moja alikuwa anaumia kwa ndani ila maumivu monomi, nashukuru Mungu yamepita na kila mmoja anaendelea na maisha mapya ndio maana nasema nafurahi kumuona akiwa katika furaha nyingine na Rotimi’- Jux

Maneno hayo aliyasema Jux wakati akihojiwa kwenye kituo cha Radio kiitwacho Kiss FM huko Nairobi nchini Kenya

Shangwe za sikukuu zimeanza DSTV wamekuja na Off kama zote itazame hii video hapa usipitwe na chochote

 

Soma na hizi

Tupia Comments