Kama ulikuja Dar es Salaam miaka kumi iliyopita na ukirudi kwasasa basi lazima ukute mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Sekta mbalimbali kuanzia Barabara, Majengo na mengineyo.
Ukiacha uboreshwaji uliofanywa kwenye sekta mbalimbali kingine ambacho kimenivutia ambacho huenda utapendezwa nacho.
Ni kuwepo na eneo jipya la wazi liitwalo Wavuvi Kempu ambalo ukutanisha watu mbalimbali wakiwemo mastaa kwaajili ya kuburudika huku kukiwa na upepo unaovuma pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
Wavuvi Kempu wanastahili pongezi na wameweza kuwa wa kitofauti na maeneo mengine ya Dar kwa huduma zao pamoja kwa ubunifu walioufanya wa kuanzisha Event iitwayo ‘Hello Jua’ ambayo ufanyika kwa mwezi mara mbili.
Najua utakuwa unajiuliza nini maana ya “Hello Jua”?
Nilipowauliza Wahusika waliniambia Hello Jua inaashiria kuchomoza kwa jua la Asubuhi ambapo Wakazi wa Dar ufika eneo majira ya saa kumi na mbili alfajiri kulisubiria Jua linavyochomoza kutokea Mashariki mwa Bahari ya Hindi.
Eneo hilo linapatikana Oysterbay Dar es Salaam kwenye yale maeneo mapya yaliyotengwa kwaajili ya kufanyia biashara kama ukiwa unaelekea Coco Beach DSM.
Bata la Wavuvi Kempu unaweza ukalifananisha na Bata la Ibiza kwani watu ujiachia na kuburudika kwa nyimbo mbalimbali.
Na Septemba 17, 2022 Wavuvi Kempu wameutangazia umma kuwa kutakuwa na Event yao pendwa iitwayo ‘Hello Jua’ ambayo wengi uisubiria Event hiyo kwa hamu kushuhudia namna watu wanavyoburudika mida ya Asubuhi.
Kwa ubunifu huu mkubwa ulifanywa na Wavuvi Kempu basi nina kila sababu ya kuwapa nyota tano mabegani kwa kuipa heshima Dar es Salaam.