AyoTV

AUDIO: Kauli ya Msuva baada ya kupokea kwa mshituko Kapombe kustaafu

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco katika club ya Difaa El Jadid Simon Msuva, ameeleza masikitiko yake kuhusiana na mchezaji mwenzake wa Taifa Stars kustaafu.

Msuva amepokea kwa masikitiko taarifa za Shomari Kapombe kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Kapombe katangaza kustaafu kucheza timu ya taifa kwa sababu ya kuwa na majeraha ya muda mrefu.

Hata hivyo Kapombe kaeleza kuwa ana imani kuwa atarejea timu ya taifa endapo tu atakuwa yuko fiti kwa asilimia 100 na kocha akiona anahitaji mchango wake.

VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete

Soma na hizi

Tupia Comments