Mix

Ndege ya Egypt imepoteza mawasiliano ikiwa na abiria kutokea Paris Ufaransa

on

EgyptAir Flight 804 imepoteza mawasiliano ikiwa angani kutokea Paris Ufaransa kwenda Cairo Misri ambako ilitakiwa kutua saa kadhaa zilizopita kwa mujibu wa CNN lakini ikapoteza mawasiliano ikiwa tayari imeingia kwenye anga ya Misri.

Shirika hilo la ndege limethibitisha kwa kusema ilikua na abiria 56 na Wafanyakazi 10 ndani yake ambapo mpaka sasa msako umeshaanza kujua ilipo ndege hii ambayo ilipotea ghafla na kutoonekana kwenye Radar.

Ramani

Ndege hii imepotea ikiwa kwenye umbali wa futi elfu 37 hewani, rubani wa ndege hiyo anao uzoefu wa kurusha ndege kwa saa 6000 huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 4000

ULIIKOSA YA MBUNGE ALI KESSY AMBAYE HATAKI VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA VIENDELEE KUJENGWA? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments