Mix

Kingine kikubwa usichokijua kuhusu wanawake wa Misri kipo hapa!!

on

465007969

Kwa wanafunzi wengi kipindi cha likizo ya mwezi wa sita ni kipindi kirefu cha likizo, ikifika wakati huo wanafunzi wengi ndio muda wa kwenda kula good time na wanafunzi wenzao kutoka shule nyingine.

Misri ni nchi ambayo unaweza ukawa unaijua kwa vitu vingi tofauti lakini ulishawahi kujua kuwa Misri ni nchi inayoongoza kwa ukeketaji wa wasichana duniani? Ripoti zinaonesha zaidi ya wasichana na wanawake milioni 125 mpaka sasa wamepitia kitendo hicho!

Kutokana na ripoti iliyotolewa mwezi wa tano na Umoja wa Mataifa, 92% ya wanawake wa Misri wenye umri wa miaka 15 hadi 49 walilazimika kupitia ukeketaji ili kukamilisha kinachoaminiwa na watu wengi kuwa ni ukamilifu wa mwanamke.

Ripoti hiyo imeonesha wasichana wengi hukeketwa kwenye umri kati ya miaka 9 hadi 12 na mara nyingi vitendo hivi hufanyika katika kipindi cha likizo ndefu ya kiangazi kila mwaka ambapo kwa huku kwetu kipindi hiki ni likizo ya mwezi wa sita mpaka nane… Japo ni kinyume cha Sheria tangu mwaka 2008 lakini bado tatizo hilo ni kubwa.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments