Habari za Mastaa

Eminem alitaka kuwadiss Kanye West na Lil Wyne?

on

Screen Shot 2014-04-02 at 2.02.30 AMEminem ambae ni msanii wa hiphop wa miaka mingi amezungumzia kitu kipya kuhusiana na wimbo wake wa ‘Talking 2 Myself’ kutoka kwenye album yake ya ‘Recovery’ iliyotoka June 2010

Anasema ni wakati ambao alijikuta kuwa ni hater tu na kwamba alitaka kuwazungumzia vibaya Kanye West na Lil Wayne ambao walikuwa mbali kimuziki time hiyo.

Namkariri akisema ‘nilikichukia kitu chochote ambacho kilikua kikipendwa (kipo hot) kwa muda ule au mtu yeyote aliekua akifanya vizuri kwa muda ule, baadae nilijiskia vibaya mimi mwenyewe na muziki niliokua nikiutengeneza kipindi hicho, nilijihisi kuanza kubadilika kuwa hater yani nikawa nachukiachukia tu watu na vitu ovyo’

Lil Wayne na Kanye West

Lil Wayne na Kanye West

Kingine cha mwisho alichosema Eminem ni kwamba angeweza kujiua kwa hali hiyo aliyokua nayo kama ya kuchanganyikiwa wakati huo, sio tu kuwachukia Kanyewest na Wayne bali kuna mengine mengi pia aliyawaza.

Tupia Comments