Baada ya kuahirishwa kwa El Clasico kwa sababu za kiusalama hatimae December 18 2019 game hiyo ilichezwa katika uwanja wa Nou Camp kwa kuzikutanisha timu vigogo wenyeji FC Barcelona dhidi ya wageni wao Real Madrid.
Game hii ilikuwa inatawaliwa na presha kubwa kutokana na timu hizo kukutana zikiwa zimefanana point hivyo mshindi wa mchezo wa leo alikuwa anaenda kukaa kileleni, game ya leo imemalizika kwa kukosa mbabe 0-0 na kuufanya msimamo wa LaLiga wafungane kwa point 36 wakicheza 17 ila Barcelona anaongoza Ligi kwa tofauti ya magoli.
Licha ya utawala wa mchezo kwa Real Madrid kwa asilimia 48 kwa 52 dhidi ya FC Barcelona waliokuwa nyumbani lakini mshambuliaji wao tegemeo Karim Benzema ameshindwa kufunga goli lake 13 LaLiga msimu huu na kuendelea kufanana na Lionel Messi ambaye nae ana magoli 12, Zidane ndio anabakiwa kuwa kocha pekee wa Real Madrid kucheza game 5 za El Clasico ugenini na kutopoteza mchezo hata mmoja.
V
AUDIO: HARUNA NIYONZIMA ANARUDI YANGA? BUMBULI KATOA JIBU