Duniani

Watu na ujasiri wao, cheki na jamaa kaiba nyoka na kumficha kwenye nguo ya ndani aliyovaa.. (+Video)

on

Hivi unaanzaje kuleta mzaha na nyoka mtu wangu ?! Eti nyoka unamuiba na bado unamficha kwenye nguo ya ndani uliyovaa ???

Mama mmiliki wa duka linalouza nyoka pamoja na wadudu wengine la A to Z Pets lililopo Portland, Oregon Marekani analalamika tu kitendo cha jamaa huyo aliyeingia kama anachekicheki hivi ahudumiwe alafu akatoka na nyoka aliyemuiba na kumficha kwenye nguo ya ndani aliyovaa.

Mama huyo Christin Bjugan amelalamika kwamba nyoka wao mwenye thamani ya kama dola 200 hivi kaibiwa na jamaa huyo, kilichosaidia akamgundua mwizi wake ni camera za CCTV alizozitega ndani ya duka lake.

Unaweza kuona tukio lote lililonaswa na CCTV mpaka jamaa anapoiba nyoka kwa kumuingiza kwenye nguo ya ndani.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments