Michezo

Kuelekea mchezo wa El Clasico kati ya Real Madrid Vs FC Barcelona, haya ni mambo matano ya kufahamu …

on

Moja kati ya michezo inayotajwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona zote za Hispania, mchezo huu ambao unaitwa El Clasico ni mchezo ambao tunaweza kuufananisha na upinzani wa Simba na Yanga. Kabla ya mchezo wao wa Jumamosi ya November 21 mtu wangu naomba nikusogezee mambo matano ya kufahamu kuelekea mchezo huo.

1- Ni mchezo unaowakutanisha wachezaji wenye rekodi ya kipekee Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, wote wanarekodi ya kuwa wachezaji pekee kuwa nominated katika kuwania tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka nane mfululizo, rekodi ambayo hakuna wachezaji waliowahi kuiweka, Messi ametwaa tuzo hiyo mara 4 na Ronaldo mara 3.

duo_3123946b

Ronaldo na Messi kila mmoja akiwa kashika tuzo yake ya Ballon d’Or

2- Hii ndio itakuwa mechi ya El Clasico ya kwanza toka mwaka 1999 kuchezwa bila uwepo wa golikipa namba moja wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas aliyetimkia FC Porto ya Ureno na kukosekana kwa kiungo wa zamani wa FC Barcelona Xavi Hernandez.

28867

Casillas na Xaxi wakisalimiana katika moja kati ya mechi za El Clasico walizowahi kukutana.

3- Klabu ya Real Madrid ndio inaongoza kuifunga FC Barcelona mara nyingi, imeifunga jumla ya mechi 92 wakati FC Barcelona wameifunga Real Madrid mara 89.

_73763932_73763931

4- Tayari Lionel Messi aliyekuwa majeruhi kwa takribani wiki nane anatajwa kuanza mazoezi na huenda akawepo katika mchezo wa El Clasico utakaochezwa November 21 kama madaktari wake watathibitisha kuwa yuko sawa kurejea uwanjani. Ila November 17 Messi alionesha kiatu chake kipya atakachochezea mechi ya El Clasico.

Lionel-Messi-boots

Kiatu ambacho kinatajwa kuwa Lionel Messi atavaa katika mechi ya El Clasico kimetengenezwa na ADIDAS

5- Messi na Ronaldo ndio wachezaji wenye rekodi ya kipekee, kwani tofauti ya umri wao ni sawa na tofauti wa umri wa watoto wao. Ronaldo ni mkubwa kwa Messi yaani amemzidi Messi siku 869, ambapo ni utofauti wa mtoto wa Messi ambaye anaitwa na Thiago na utofauti wa mtoto wa Ronaldo anayeitwa Cristiano Ronaldo Junior ambapo yeye pia ni mkubwa kwa mtoto wa Messi kwa siku 869.

6057156223960338_20779271aa1c14ea9a0610f309660daf5c8c2c6a80e1f69f27ed706f81fe23ef_large

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments