Kamishna wa Elimu Tanzania, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema elimu inayotolewa na Jumuiya ya Montessori hapa nchini inamanufaa kwa jamii kwani imejikita katika kuwaelimisha watoto katika umri mdogo.
Akifungua kongamano la 26 la Jumuiya yaMontessori Tanzania Dkt. Mtahabwa amesema Jumuiya hiyo inafanya kazi kubwa katika kutoa elimu kwa watoto wa kitanzania na kwamba umefika wakati elimu hiyo imepewe kipaumbele.
Kamishna huyo wa elimu amesema ni jukumu la Jumuiya hiyo ya Montessori kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa “ku-Connect” na watoto wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Montessori Sarah Kiteleja amesema Mazingira ya Montessori yanamwandaa mtoto tangu anapozaliwa hadi umri wa miaka 6 na wanalindwa na kupata elimu bora.