Mmiliki wa Twitter, Elon Musk amefichua mipango yake ya kuajiri Makamu wa Rais wa Uchawi na Propaganda kwenye mtandao wake na alisema tayari ameanza kutafuta mtu ambaye angefaa nafasi hiyo.
Tajiri huyo mkubwa zaidi duniani alifichua hayo katika ujumbe wake wa Twitter Jumapili usiku baada ya Megan Fox kujiita ‘mchawi’ katikati ya mabishano kwenye mitandao ya kijamii na mchambuzi wa kihafidhina Robby Starbuck, ambaye alikosoa jinsi mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anavyolea watotot wake watatu.
Story ya Elon kuhusu uchawi pia inaambatana na kitu ambacho Megan alichapisha baada ya taarifa yake ya IG. aliweka picha kutoka kwenye makala ya habari mapema wiki hii ambayo inadaiwa kuwa alinasa picha za “wachawi” wa maisha halisi wakila mzoga wa kulungu nje ya shamba video iliyyo shtua wengi na kusambaa sana mtandaoni.
Aliandika, “Natafuta kuajiri VP wa Witchcraft & Propaganda.
“Looking to hire a VP of Witchcraft & Propaganda
Elon Musk mwezi uliopita alimtangaza Linda Yaccarino kama Afisa Mkuu Mtendaji mpya wa Twitter na sasa anamtafuta mchawi wa kusimamia shughuli nyingine.
Hivi majuzi zilisambaa tuhuma za kukasirisha za unyanyasaji wa watoto dhidi ya Megan Fox ambazo zilikuzwa na Elon Musk kwenye Twitter.
Muigizaji huyo alishtakiwa kwa unyanyasaji wa watoto kwa madai ya kuwalazimisha wanawe kuvaa nguo za wasichana.
Madai hayo yalitolewa na mkurugenzi na mtayarishaji Robby Starbuck ambaye alishare picha ya mwigizaji huyo na watoto wake na kuandika, “Hawa ni watoto wa Megan Fox. Tulikuwa tunaishi pamoja na watoto wetu walicheza kwenye bustani. Niliona habari kuhusu watoto kulazimishwa na mama yao kuvaa nguo za wasichana huku yaya wao akijaribu kuwafariji. Ni unyanyasaji mtupu wa watoto. .”
Kumbuka, anapendekeza kwamba anahitaji kuajiri mtu ili kuchuja propaganda na uchawi kwenye Twitter .