Habari za Mastaa

BAADA YA NDOA: Mbasha alipoulizwa kuhusu uwezo wa Flora kuimba

on

Mume wa zamani wa Florance Henry (zamani Flora Mbasha) ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha usiku wa May 5, 2017 kupitia TV show ya SHILAWADU amehojiwa na kuzungumza kwa mara ya kwanza toka Flora afunge ndoa na Mume mpya Mwanza. 

Kwenye Interview hiyo Emmanuel amesema pamoja na mambo mengine, bado Flora ni mwimbaji mzuri kwenye muziki wa Injili >>> “Flora kama Flora ni mwimbaji mzuri, anajua kuimba,  amebarikiwa kuimba, haya mengine ni mapungufu tu hakuna asiyejua kama Flora anaweza kuimba, kipindi anaimba nilikuwa namtanguliza sana yeye’ 

“Mimi sikuwa na nyimbo wala album wala chochote kwa hiyo mwimbaji alikuwa ni yeye, mimi nilikuwa nasimamia kitu kikae sawa na kuhakikisha kitu hakikwami….. watu walituona sana tumeimba sana kwenye kampeni.”Emmanuel Mbasha.

EXCLUSIVE: Flora awajibu wanaosema kamzidi kiumri Mume mpya na kuhusu kumualika Mume wake wa zamani kwenye harusi.

EXCLUSIVE VIDEO: Mume mpya wa Flora afunguka baada ya ndoa, mtazame kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments