Mix

Bendera ya Marekani ilivyoshuhudiwa inapepea Cuba kwa mara ya kwanza baada ya miaka 54 kupita…

on

_84898182_028556400-1

Ni August 14 2015 inaandikwa Historia nyingine kubwa Duniani, Marekani na Cuba ni nchi ambazo hazikuwa kwenye uhusiano mzuri kwa muda mrefu, imeshuhudiwa kwa mara ya kwanza toka mwaka 1961 bendera ya Marekani imepandishwa kwenye Ubalozi wa Marekani Cuba kumaanisha kwamba sasa hivi kila kitu kinaelekea kuwa sawa kati ya nchi hizo mbili.

John Kerry anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Marekani kutembelea Cuba ndani ya kipindi cha miaka 70, yeye pamoja na baadhi ya Wanajeshi wastaafu wa Marekani wameshuhudia tukio hili la kihistoria kwenye Ubalozi wa nchi hiyo ulioko Jiji la Havanna, Cuba.

_84899792_028557109-1

Katibu Mkuu wa Marekani, John Kerry akiwa na mmoja ya Wanajeshi Wastaafu walioshusha bendera ya Marekani mwaka 1961 Cuba.

Historia hii inaandikwa ikiwa ni miezi nane toka Marekani na Cuba wamekubaliana kumaliza tofauti zao Kidiplomasia, Cuba wao walipandisha Bendera yao kwenye Ubalozi wao ulioko Washington Marekani July 20 2015.

Tuko kwenye majadiliano na Cuba kwamba waweke mfumo mzuri wa Utawala wa Kidemokrasia ambapo watu watakuwa na uhuru zaidi kuchagua Viongozi wao“– John Kerry.

Mbuzi

Mwezi December 2014 Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Raul Castro wa Cuba walikubaliana kurudisha uhusiano mzuri pamoja na kufungua Balozi za nchi zao ili kuurudisha ukaribu wa uhusiano wa nchi zao ambao haukuwa mzuri kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

_84898180_028556640-1

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments