Maajabu

Jamaa kanywa energy drinks nane… Baada ya hapo ni habari…

on

energy drink cansHivi umeshawahi kukutana na watu wanashindana kufanya kitu fulani cha kawaida tu, kama kula ama kunywa… ama chochote kile, halafu mwisho wa mabishano hayo wanawekeana hata hela ili atayayemshinda mwenzake anachukua kiasi chote cha pesa ambacho kimewekwa.

Huyu aliwekewa pesa kiasi cha Naira 1,600 za Nigeria na kuambiwa iwapo angemaliza chupa nane za energy drink angekuwa amejishindia kiasi hicho cha pesa kutoka kwa Chikwado Nchionu.

Elijah Nwankwo alipatwa na umauti huo wakati akifanya jitihada za kushinda pesa hizo, ambapo kifo chake kimethibitika kuwa kilitokana na kunywa kwa wingi kinywaji hicho huko Nigeria.

Walioshuhudia wanasema baada ya kunywa kinywaji hicho aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu, baada ya kumfikisha Hospital akawa ameshafariki.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments