Michezo

England wameomba Jumatatu iwe mapumziko wakitwaa Euro 2020

on

Mashabiki zaidi ya 100,000 wa England wamesaini petition ya kuomba serikali ya Uingereza itangaze Jumatatu July 12 iwe siku ya mapumziko endapo England watatwaa Ubingwa wa Euro 2020.

England wanacheza na Italia Jumapilii ya July 11 hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua ya fainali ya Euro lakini ndio wanafanikiwa kufika fainali ya michuano mikubwa kwa mara ya kwanza toka 1966 walipotwaa Kombe la Dunia.

England hawajapata matokeo chanya dhidi ya Italia katika mechi zao nne za mwisho walizokutana katika michuano mikubwa, huku England wakiwa hawajawahi kupoteza mchezo wowote wa mashindano makubwa katika uwanja wao wa Wembley.

Soma na hizi

Tupia Comments