Michezo

CAF yafuta matokeo ya fainali ya Club Bingwa Afrika

on

Shirikisho la soka Afrika CAF baada ya kukaa kikao cha dharura Paris Ufaransa kimekuja na majibu ya kufuta matokeo ya michezo yots miwili ya fainali ya CAF Champions League kati ya Wydad Casablanca dhidi ya Esperance.

Kutokana kufutwa kwa matokeo hayo club ya Esperance ya Tunisia italazimika kurudisha taji hilo pamoja na medali za ubingwa za wachezaji wake walizokuwa wamepewa baada ya wachezaji wa Wydad kugoma kuendelea na game.

Mchezo huo wa fainali utachezwa baada ya fainali ya AFCON, kama utakuwa unakumbuka vizuri Esperance alipewa Ubingwa kufuatia wachezaji wa Wydad kugoma kuendelea na mchezo baada ya goli lao kukataliwa dakika ya 59 na muamuzi Bakary Gassama kutokea Gambia kugoma kwenda kuangalia uhalali wa goli hilo kupitia VAR.

Soma na hizi

Tupia Comments