Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

EPL: Unadhani Man United wameweza kulipiza kisasi kwa Leceister? Cheki matokeo hapa

on

IMG_1311-1.PNG

Kumbukumbu za mchezo wao uliopita, Louis Van Gaal anasema ni kitu ambacho angependa kukisahau, wakiwa wanaongoza kwa magoli 3 mechi ikaishia kwa kufungwa 5-3 na Leicester City.

Leo hii miezi takribani minne tangu mechi hiyo ya kwanza ya EPL kuchezwa, Leceister walisafiri mpaka jijini Manchester kwenda kucheza na Man United.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford umemalizika kwa Louis Van Gaal kuiongoza United kuweza kulipa kisasi kwa kuifunga Leceister kwa magoli 3-1.

Magoli ya United yalifungwa na Van Persie, Radamel Falcao na moja la kujifunga kwa Leceister wenyewe.

Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko United walikuwa wanaongoza 3-0.

Kipindi cha pili United walipunguza kasi na Leceister wakajaribu kufanya maajabu ya kusawazisha magoli na hata kupata ushindi kabisa lakini siku haikuwa yao, wakaishia kupata goli moja tu lilofungwa na Wasilewski.

Man U

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter,  Instagram  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments