Michezo

EPL kama Tanzania wazuia wachezaji kupeana mikono

on

Ligi Kuu England wamezuia wachezaji na waamuzi kusalimiana kwa kupeana mikono kuanzia mechi za weekend hii hadi watakapopewa taarifa nyingine, hii inakuja kutokana na hofu ya virusi vya corona.

Taarifa za EPL kutangaza hivyo zinakuwa za pili baada ya siku moja nyuma shirikisho la soka Tanzania TFF kutangaza zuio kama hilo kwa wachezaji na waamuzi kutosalimiana kwa kupeana mikono.

Mwaka 2014 chuo kikuu cha Aberystwyth cha nchini Wales kwa mujibu wa tafiti ilizozifanya, ilibaini kuwa kusalimiana kwa kupeana mikono kunasambaza bakteria mara 2 zaidi ya ya kusalimiana kwa kupeana tano.

 

Soma na hizi

Tupia Comments