Michezo

EPL: Matokeo ya Chelsea vs West Brom na rekodi ya Fabregas

on

IMG_8982.JPG

Viongozi wa ligi kuu ya England klabu ya Chelsea leo wamekutana na klabu ya West Brom – timu ambayo katika mechi 5 zilizopita kabla ya leo, The Blues walikuwa wamefanikiwa kupata ushindi mara moja tu.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye dimba la Stamford Bridge imemalizika kwa vijana wa Jose Mourinho kuendelea kuchanua kwenye uongozi wa ligi kwa kupata pointi 3 dhidi ya West Brom.

Mfungaji bora wa timu hiyo mhispania Diego Costa alifunga goli la kwanza katika dakika ya 11 ya mchezo kabla ya Eden Hazard kufunga mahesabu dakika 14 baadae kwa kufunga goli zuri katika dakika ya 25.

Wakati huo huo kwenye mchezo huo Cesc Fabregas ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha pasi za magoli 10 kwa haraka zaidi kwenye ligi ya England tangu ilipoanzishwa.

Chelsea sasa wamefikisha pointi 32 kutoka kwenye michezo 12 ya ligi hiyo.

TAKWIMU ZA MCHEZO

Chelsea (4-2-3-1): Courtois 6; Ivanovic 7.5, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7; Fabregas 8.5, Matic 7.5; Willian 7 (Ramires 86), Oscar 8 (Remy 79, 6), Hazard 8; Costa 8 (Drogba 83)
Subs not used: Cech, Luis, Zouma, Schurrle
Booked: Willian
Manager: Jose Mourinho 8
West Brom (4-2-3-1): Foster 8; Wisdom 6, Lescott 6, Dawson 5.5, Baird 5.5 (Gamboa 68, 5); Yacob 4, Gardner 6; Dorrans 6 (Morrison 84), Sessegnon 6, Brunt 5; Berahino 6 (Anichebe 78, 5)
Subs not used: Myhill, Ideye, McAuley, Samaras
Booked: None
Sent off: Yacob
Manager: Alan Irvine 6
Referee: Lee Mason 6.5
Man of the match: Cesc Fabregas
Attendance: 41,600

Tupia Comments