Kocha wa Manchester United Erik ten Hag ameripotiwa kuwataka Mashetani Wekundu hao kumsajili chipukizi wa Brazil Estevao Willian, ambaye pia yuko kwenye rada za Real Madrid, Chelsea na Barcelona.
Kwa mujibu wa ripoti ya Fichajes, Man United pia wanataka kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 16, ambaye kwa sasa anaichezea Palmeiras.
Ongezeko la hivi majuzi la Man United kwenye safu ya winga, Antony na Jadon Sancho, limeshindwa kuacha athari kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Hata hivyo, kikosi hicho cha Ten Hag pia kitalazimika kushindana na vilabu vya Real Madrid, Chelsea na Barcelona kuwania saini ya Willian.
Willian alifunga mabao matatu na kutoa idadi sawa ya asisti katika mechi tano kwenye Kombe la Dunia la FIFA la U-17 2023 kabla ya Selecao kuondolewa na Argentina katika robo fainali mnamo Novemba 24.