Michezo

Usisahau kwamba Chelsea imecheza February 13, wamempa mtu 5

on

Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena leo February 13 kwa jumla ya michezo 7 kupigwa katika viwanja kadhaa Uingereza, Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo ambao msimu huu wamekuwa wakisuasua kupata matokeo mazuri, klabu ya Chelsea The Blues walikuwa wenyeji wa Newcastle United katika dimba la Stamford Bridge.

4928

Klabu ya Chelsea ambayo bado ipo chini ya kocha wa muda Guus Hiddink imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya goli 5-1 dhidi ya Newcastle United, ushindi ambao umewafanya wafikishe jumla ya point 33, wakiwa nafasi ya 12 katika michezo yao 26 waliocheza katika Ligi Kuu msimu huu, ushindi huo umekuja wakati ambao Chelsea ilidumu kwa nafasi ya 13 kwa wiki kadhaa.

4397

Magoli ya Chelsea yalianza kufungwa dakika ya 5 na Diego CostaPedro Rodriguez dakika ya 9, Willian dakika ya 17, Pedro Rodriguez tena dakika ya 59 na Bertrand Traore akapiga goli la tano dakika ya 83, Newcastle United walipata goli la kufutia machozi dakika ya 90 kupitia kwa Andros Townsend. hivyo mchezo ulimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 5-1, huku Newcastle United ikibaki  kushika nafasi ya 18 kwa kuwa na point 24 katika michezo yao 26 ya Ligi.

2365

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa February 13

  • Sunderland 2 – 1 Manchester United
  • Crystal Palace 1 – 2 Watford
  • Everton 0 – 1 West Bromwich Albion
  • Norwich City 2 – 2 West Ham United
  • Swansea City 0 – 1 Southampton
  • AFC Bournemouth 1 – 3 Stoke City

Video ya magoli ya mechi ya Chelsea Vs Newcastle United

https://youtu.be/DRm7xN43s9w

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments