Michezo

Hali mbaya Man United yakubali kipigo kwa Bournemouth, Cheki matokeo ya EPL Dec 12 (+Pichaz&Video)

on

Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena leo December 12 kwa mechi takribani sita kupigwa katika ardhi ya Malkia Elizabeth, miongoni mwa michezo iliyochezwa Jumamosi ya December 12 ni AFC Bournemouth dhidi ya klabu ya Manchester United inayofundishwa na kocha wa kiholanzi Louis van Gaal.

4079

Mchezo huo ambao Man United walikuwa ugenini ulimalizika kwa Man United kukubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa wenyeji wao AFC Bournemouth. Ikiwa huu ulikuwa mchezo wa 16 kwa Man United ambayo inashika nafasi ya nne katika Ligi ikiwa na point 29, imefikisha jumla ya mechi tatu ilizopoteza msimu huu.

2000

Mchezo ulianza kwa AFC Bournemouth kupata goli la mapema tu, kwani dakika ya 2 Junior Stanislas alifunga goli la kwanza kwa AFC Bournemouth kabla ya dakika ya 24  Marouane Fellaini kuisawazishia Man United na kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1. Kipindi cha pili  AFC Bournemouth walikuja na kasi na kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 54 kupitia kwa Joshua King.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza December 12

  • Norwich City 1 – 1 Everton
  • Crystal Palace 1 – 0 Southampton
  • Manchester City 2 – 1 Swansea City
  • Sunderland 0 – 1 Watford
  • West Ham United 0 – 0 Stoke City

Video ya magoli ya AFC Bournemouth Vs Man United

https://youtu.be/3y0o9TerHLQ

Video ya magoli ya Man City Vs Swansea City

https://youtu.be/PSf14jZoHMQ

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments