Baada ya wapinzani wao Man United kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford, Man City walisafiri kutoka jiji la Manchester hadi London kuwafuata wagonga nyundo wa London West Ham United, mchezo ambao umepigwa katika dimba la Olympic Stadium.
Man City nusura wachezee kichapo kutoka West Ham United, pongezi nyingi ziende kwa muargentina Sergio Aguero ambaye alifanikiwa kuiokoa Man City dakika ya 81 ikiwa nyuma kwa goli 2-1, baadaya kupachika goli la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tisakabla ya mchezo kumalizika.
West Ham United ndio walikuwa wa kwanza kupachika goli la kwanza dakika ya 1 Enner Valencia, goli ambalo lilidumu kwa dakika nane tu, kwani dakika ya 9 Man City walipata penati iliyopigwa na Sergio Aguero na kutinga nyavuni, Enner Valencia alirudi tena nyavuni dakika ya 56 na kupachika goli la pili, lakini dakika ya 81 Sergio Aguero alisawazisha na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya goli 2-2.
https://youtu.be/CzbBykcEVPY
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.