Michezo

Man United VS Aston Villa.. Hivi nd’o ilivyokua jana mtu wangu..

on

Ligi kuu ya England imeendelea tena jioni ya leo baada ya kupisha mechi za kimataifa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Manchester United baada ya kupata matokeo ya ushindi dhidi ya wapinzani wao wa jadi Liverpool wiki mbili zilizopita, leo hii walikuwa katika dimba lap la nyumbani kucheza dhidi ya Aston Villa.

Villa waliingia Old Trafford wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya United katika raundi ya kwanza ya EPL, lakini leo hii hali ilikuwa tofauti wakicheza na United ambayo ipo katika kiwango cha juu.

Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 3-1 kwa vijana wa Louis Van Gaal.

Magoli ya Ander Hererra aliyefunga mawili na Wayne Rooney aliyefunga moja yalitosha kuipeleka United mpaka nafasi ya 3 katika msimu wa ligi mbele ya Man City ambao watakipiga na Crystal Palace jumatatu usiku.

Man U itakairibisha City Old Trafford wikiendi ijayo katika mchezo wa raundi ya pili ya EPL.

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments