Beki wa kati wa Simba SC Erasto Nyoni baada ya Timu ya Majimaji ya Songea kukwama jijini Dar es Salaam kwa kukosa pesa ya nauli na deni la hotel jana alifanikiwa kuwasaidia kulipa na kuwapa Tsh milioni moja ambayo wamefanya nauli ya kurejea Songea.
Erasto ni mwenyeji wa Songea na amezungumza na Ayo TV kwa njia ya simu na kueleza kuwa amewahi kupita hali kama hiyo, hivyo ameamua kuwasapoti ili kuwatia moyo.
“Sisi kama kaka zao tunatakiwa tuwaoneshe na tuwape moyo ili waweze kupambana maana kazi yetu ya mpira ni kazi ngumu sana unatakiwa usikate tamaa uwe mvumilivu sasa uvumili hauji tu hivi hivi lazima kuna watu wawe wanakupa hiyo nguvu”
“Nimeshawahi kupitia hii hali ndio maana ilipotokea ikanisukuma ikanisukuma kufanya hivi sababu ishawahi kunitokea”>>> Erasto