Michezo

Eriksen kafuzu vipimo vya afya Inter Milan

on

Kiungo wa Tottenham Hotspurs Christian Eriksen amefuzu vipimo vya afya na sasa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake wa kutoka Tottenham kujiunga na Inter Milan.

Eriksen amefuzu vipimo vya afya baada ya kukamilisha zoezi hilo usiku wa leo, hivyo anajiandaa kusaini mkataba wa kuitumikia Inter Milan kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 17.5, utakaomuwezesha kulipwa pound 130,000 kwa wiki kabla ya kodi.

Taarifa zinaeleza kuwa staa huyo wa Denmark atasaini mkataba wa miaka minne na nusu kuitumikia Inter Milan, Eriksen aliwasili Tottenham 2013 kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 11 akitokea Ajax.

Soma na hizi

Tupia Comments