Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ imetangaza kuongeza kwa mara nyingine muda wa kulipa kodi ya majengo ambayo kwa Mwaka Fedha 2016/17 na sasa muda wa mwisho utakuwa July 31, 2017.
Awali TRA iliongeza muda wa kukusanya kodi hizo ambao siku ya mwisho ilikuwa leo July 15, 2017 lakini kutokana na mwamko mkubwa kwa Watanzania katika kulipa kodi hiyo Mamlaka hiyo imelazimika kuongeza hadi July 31, 2017 ili kutoa nafasi zaidi kwa Watanzania kulipa.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema:>>>“Tunatambua kuna watu ambao hawajaweza kufanya hivyo. Hivyo tunachokifanya ni kwamba ili tusiathiri kodi zingine ambazo zinaendelea kukusanywa kwa sababu katika kipindi hiki staff wetu walijikita zaidi kwenye kodi ya majengo na wakati huo huo tulisimamisha kukusanya kodi za mwaka huu za majengo.
“Sasa ili vyote viende kwa pamoja na kwa utaratibu mzuri na kutowanyima nafasi ambao wanataka kuendelea kulipa kodi za mwaka huu tumeona kwamba tuweke vituo maalumu na tuendelee kuwahudumia mpaka mwisho wa mwezi.” – Richard Kayombo.
TRA Mwanza siku moja kabla ya muda wa mwisho kulipia kodi ya majengo!!!