Club ya Espanyol na Leganes zimetangaza njia mbadala ya kupunguza hasara kwa club na mashabiki wake waliokuwa wamekata tiketi za msimu 2019/20 wakati huu ambao kuna mlipuko wa janga la Corona.
Kwa pamoja Espanyol na Leganes wametangaza kuwa litawafidia mashabiki zake kwa kuingia bure msimu wa 2020/21 kwa wale waliokuwa wamekata tiketi za msimu sababu msimu huu ambao utaendelea June utamaliziwa kwa kuchezwa bila mashabiki.
Hadi Ligi Kuu ya Hispania LaLiga msimu wa 2019/20 unasimama mwezi March sababu ya janga la Corona mashabiki hao walikuwa washataza asilimia 20 ya mechi za nyumbani za timu yao kwa waliyokata tiketi za msimu.