Habari za Mastaa

Essence ya Wizkid yapeta kwenye charts za Billboard hot 100, yakamata nafasi hii

on

NI Headlines za wimbo wa mkali kutokea Nigeria Wizkid uitwao Essence ambao ameshirikisha mrembo Tems ambapo time hii umetajwa kuingia katika charts kubwa za Billboard Hot 100.

Wimbo hut umefanikiwa kushika katika nafasi ya 82 kwenye charts hizo za Billboard na unaambiwa hii inakuwa ni mara ya tatu kwa star huyo kuingia kwenye rekodi hizo ambapo mwaka 2016 kibao chake kinachofahamika kwa jina la One Dance ilifanikiwa kushika namba 1 na Mwaka 2020 aliweka rekodi ya pili kupitia wimbo wake uitwao Brown Skin Girl ambapo ulishika namba 76.

kwa hiyo rekodi hizo zinamuweka kwenye nafasi nzuri ya muziki na kwa upande wa mrembo Tems inakuwa ni mara yake ya kwanza kuingia kwenye charts hizo za Billboard hot 100.

Na kwa upande wa Youtube tangu iwekwe mwezi April 9 imeweza kutazamwa na watu zaidi 13,774,070.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tupia Comments