Uchaguzi wa wabunge unaafanyika Ijumaa hii nchini Eswatini, zamani ikiitwa Swaziland, nchi ya mwisho barani Afrika iliyo chini utawala wa kifalme wenye nguvu.
Baadhi ya wapiga kura 585,000 waliojiandikisha wameitishwa kuchagua wabunge 59 wa Bunge. Isipokuwa kwamba vyama vya siasa havijaidhinishwa kushiriki katika kupiga kura na kwamba Bunge lina jukumu la kushauriana tu.
Hii ni kura ambayo haitabadili hali ilivyo nchini Eswatini. Mfalme Mswati 3 ana mamlaka yote kabisa. Anaidhinisha rasimu zote za sheria na anatumia katika maamuzi yake kura ya turufu. Bunge lina jukumu la ushauri tu.
Zaidi ya hayo, wagombea hawawezi kuwakilisha chama cha siasa. Waliteuliwa wakati wa kura za mchujo mwezi uliopita na wengi wao ni waaminifu kwa mfalme. Ni wagombea dazeni pekee wanaojulikana kuwa katika upinzani.
Moja ya vyama vikuu vya upinzani, Pudemo, kilipigwa marufuku rasmi na mamlaka na kuitwa kundi la kigaidi.
Nchi imetawaliwa kwa mkono wa chuma kwa miaka 37 na Mfalme Mswati 3. Mwenye mamlaka yote, anaweza kuvunja Bunge na serikali, kuteua au kufukuza majaji. Pia anaamuru polisi na jeshi.
Katika miaka ya hivi karibuni, hata hivyo, ufalme huo umetikiswa na maandamano ya kuunga mkono demokrasia, ambayo yalikandamizwa kwa nguvu zote.