Mix

Yusuph Jackson ndio jamaa aliyeshinda Renault Kwid

on

 

Mkazi wa Serengeti, Mugumu Bwana Yusuph Jacksoni Murimi(29) akabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid mara baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Faidika na Jero.

 

Promosheni ya Faidika na Jero ilidumu kwa siku 40 ambapo watumiaji wa mtando wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo smartphone kila siku nasiku ya mwisho zawadi ya gari.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano Yusuph alisema” Ukirudia mazungumzo yangu siku ya kwanza wakati napigiwa simu utagundua kwamba nilikuwa siwaamini walionipigia simu kama ni kweli SportPesa maana siku hizi mjini watu hawatabiriki. Nilikuwa nacheza tu lakini sikutarajia bahati hii ya ushindi wa gari itanidondokea mimi”

 

“SportPesa wamenipa mapokezi mazuri ikiwemo kusimamia gharama zote kuanzia usafiri wa ndege, malazi pamoja na matumizi ya siku nzima  na kuhakikisha gari langu linapata usajiri kupitia jina langu na kukabidhiwa”

 .

“Sijui nisemeje lakini nawashukuru sana SportPesa, Mimi ni muajiriwa kwenye kampuni kama fundi welder na sikutarajia kama siku ningeweza kushinda zawadi ya gari”

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas alisema “SportPesa inazidi kuwafungulua dunia wateja wake hasa kwa kupitia promosheni mbalimbali kupitia simu ya mkononi unaweza kufanya maajabu yanayoweza kubadili maisha yako.”

.

 “Napenda kumpongeza sana sana Bwana Yusuph kwa ushindi wake na kujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwid na kuweza kuitumia kujiingizia kipato na shughuli nyingine za kujenga taifa.”

 .

“Hivyo basi watanzania wakae mkao wa kula mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka SportPesa ili kuwaongezea burudani wateja wetu”

 

 

Tupia Comments