Vikosi vya serikali ya Ethiopia viliwaua wakazi wasiopungua 45 wa mji moja katika jimbo la Amhara (kaskazini) mnamo Januari 29, ambapo walipambana na wanamgambo wa eneo hilo, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) imeshutumu leo Jumanne.
Taasisi ya umma inayojitegemea kisheria, EHRC inazingatia katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba tathmini hii iko chini ya ukweli kwa sababu, kushindwa kuwa na uwezo wa “kukusanya taarifa kamili kutokana na hali ya usalama” hasa, “kazi yake ya uchunguzi haikuweza kufanyika kikamilifu.
EHRC inaeleza kuwa inachunguza “wahanga wa kiraia kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama vya serikali na Fano”, wanamgambo wa Amhara, mnamo Januari 29, 2024 huko Merawi, eneo la takriban kilomita 30 kusini mwa mji mkuu wa mkoa wa Bahir Dar.
“Kulingana na uchunguzi wa kina, ukaguzi uliofanywa na EHRC ulifanya iwezekane kuthibitisha utambulisho wa angalau raia 45 waliouawa na vikosi vya usalama vya serikali, kwa sababu walituhumiwa kuunga mkono Fano,” inabainisha taasisi hiyo.