AyoTV

Sentensi 5 za walichosema Samuel Eto’o na Davido London, pia tazama wakicheza skelewu

on

Screen Shot 2014-04-12 at 1.47.20 PMMwanzoni ilitoka video ya sekunde chache ikionyesha jinsi Davido anamfundisha Samuel Eto’o jinsi ya kucheza Skelewu lakini hii ni full interview kutoka kwenye Youtube channel ya Samuel Eto’o ambapo wanafanyiwa interview wakizungumza mambo mbalimbali.

  1. Davido anasema alifurahi kukutana na Eto’o ambae toka akiwa mdogo alikua ana muona kwenye TV akicheza football ambapo sasa muziki ndio umempa nguvu na kumkutanisha na Eto’o.
  2. Staa huyu wa Nigeria anasema alianza kidogokidogo kwenye muziki ambao umekuja kumpa mafanikio na pesa ya kuweza kununua nyumba zake pamoja na magari kitu ambacho kiliishawishi familia yake kujua muziki una hela na wakawa na furaha na anachokifanya.
    11113. Eto’o amesema alizaliwa kwenye familia masikini lakini yenye maadili na misingi bora ya kumkuza mtoto ambapo pamoja na utajiri na umaarufu alionao kwa sasa, bado amekua ni mtu wa kujishusha na kuwa kwenye level moja na wengine na haoni sababu ya pesa kumbadilisha kitabia.

  3. Staa huyu wa soka kutoka Cameroon anaamini ni haki yake kurudisha kwa jamii ndio maana ni mipango yake kujenga hospitali kwa ajili ya watu wasio na uwezo kifedha kutibiwa.

  4. Kwa kumalizia, Davido amesema hana ushindani na P Square na anawaheshimu kama kaka zake waliomtangulia kwenye muziki hivyo hakuna ushindani, wote wanatengeneza hela tu.

Unaweza kutazama interview nzima kwenye hii video hapa chini.

[youtube youtubeurl=”–9H5S8C-S4″ ][/youtube]

Unataka kila tukio linalonifikia niwe nakutumia? karibu ujiunge na familia ya millardayo.com kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ambapo iwe usiku au mchana nitakutumia chochote kinachonifikia.

Tupia Comments