Michezo

Eto’o apata ajali ya gari Cameroon

on

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na club ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o ameripotiwa kupata ajali nchini Cameroon.

Eto’o amepata ajali ya gari akitokea katika mji wa Bafoussam alikokuwa kaenda kwa ajili ya kuhudhuria harusi lakini alipokuwa njiani akirejea katika mji wa Douala ndio akapata ajali hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari Cameroon na Afrika Magharibi kwa ujumla vinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo Eto’o alipelekwa hospitali na hali yake ni nzuri alipata majeraha madogo.

Soma na hizi

Tupia Comments